MUDAVADI AANZA ZIARA MAREKANI KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI KWA WAKENYA
Katika juhudi za kuwafaidi Wakenya kiuchumi na kuimarisha nafasi ya Kenya kimataifa, Waziri Mkuu Musalia Mudavadi ameanza ziara rasmi mjini Washington, Marekani, kufuatia mwaliko wa serikali ya Marekani.
Mudavadi anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio na Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Kigeni Brian Mast, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara, usalama na uwekezaji.
Pia atakutana na wawekezaji kupitia kongamano la biashara katika US Chamber of Commerce, hatua inayolenga kufungua fursa mpya za ajira na kukuza uchumi wa Kenya kupitia uwekezaji wa kimataifa.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































