STEPH CURRY AONGEZA MKATABA NA GOLDEN STATE WORRIORS

Mchezaji Nyota wa timu ya Golden State Warriors Stephen Curry amekubali kuongezewa mwaka mmoja kwenye mkataba wake kwa mshahara wa $62.6 milioni (Ksh 8 billion) ili aendelee kusalia na Golden State hadi msimu wa 2026-27.
ESPN iliripoti kwamba wakala wa Curry, Jeff Austin, alikuwa amethibitisha dili hiyo kwa mchezaji huyo bora mara mbili wa NBA.
Curry, 36, alikuwa na miaka miwili iliyosalia kwenye mkataba wa miaka minne, wa dola milioni 215.4 aliotia saini Agosti 2021.
Kulingana na “sheria ya zaidi ya mkataba kwa mchezaji mwenye umri zaidi ya miaka 38” katika makubaliano ya pamoja ya mazungumzo, alistahili tu kuongezewa mwaka mmoja msimu huu wa nje ya umri huo.
Kwa sababu atafikisha miaka 38 wakati wa mwisho wa mkataba uliokuwepo (Machi 14, 2026).
Imetayarishwa na Janice Marete