#uncategorized

SERIKALI ITAGHARAMIKA SHILINGI BILIONI 30 KUKARABATI BARABARA

Waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen amesema serikali itagharamika kati ya shilingi bilioni 25 hadi bilioni 30 katika kukarabati miundomsingi ya uchukuzi iliyoharibiwa na mafuriko.

Akizungumza katika kaunti ya Lamu alikozuru kutathmini barabara zilizoharibika katika kaunti hiyo, Waziri Murkomen amekiri kutatizika kwa hali ya usafiri kote nchini kutokana na mafuriko.

Amesema kwamba nyingi ya miundomisingi iliyoathirika zaidi ni daraja.

Imetayarishwa na: Antony Nyongesa

SENETI YAMHOJI WAZIRI MVURYA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *