#Local News

WIZARA YA AFYA YAFANYA MAZUNGUMZO NA BARAZA MAGAVANA LA AFYA KUEPUSHA MGOMO WA MADAKTARI

Utoaji wa huduma za afya katika hosipitali za umma unatarajiwa kuathirika iwapo madaktari watashiriki mgomo tena ikiwa mkataba wa makubaliano uliotiwa saini hivi majuzi hautazingatiwa.

Wizara ya afya in asema kuwa itashirikiana kwa karibu na baraza la magavana nchini, kuepusha mgomo huo wa madaktari.

Akiongea alipomtembelea mwenyekiti wa kamati ya baraza la magavana kuhusu afya Muthomi Njuki kwenye makao makuu ya baraza hilo, waziri wa afya Deborah Barasa amesema wizara hiyo itatekeleza makubaliano hayo kwa wakati ufaao ili kuzuia mgomo huo.

Ameongeza kuwa wizara yake itashughulikia pendekezo la magavana la kutaka kulipwa kwa fedha za wahudumu wa afya ya jamii kutoka kwa hazina moja.

Kwa uapande wake, Muthomi Njuki ametoa wito kwa wizara ya afya kutumia njia zote kuhakikisha mgomo wa madaktari unaepushwa.

Katika mkutano huo, baraza la magavana limetoa wito wa ushirikiano bora na wizara ya afya, likilalamikia kutengwa katika utoaji maamuzi muhimu, huku likiarifiwa katika dakika za mwisho kuweka muhuri kile ambacho kimekubaliwa na wizara ya afya.

Imetayarishwa na Janice Marete

WIZARA YA AFYA YAFANYA MAZUNGUMZO NA BARAZA MAGAVANA LA AFYA KUEPUSHA MGOMO WA MADAKTARI

MBEGU, MBOLEA GHUSHI HATARI- WATAALAMU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *