#Business

SERIKALI YAPUNGUZA BAJETI YA MWAKA WA KIFEDHA

Hazina ya Kitaifa imetangaza marekebisho ya bajeti ya matumizi ya kawaida kwa mwaka wa kifedha wa 2025/2026, ikipunguza bajeti hiyo kwa takriban shilingi bilioni 10. Kulingana na ripoti ya Business Daily, bajeti hiyo sasa inasimama kwenye shilingi trilioni 1.73, ikiwa ni sehemu ya hatua za serikali kupunguza matumizi.

Hatua hii inafuatia uamuzi wa Baraza la Mawaziri kupitisha kupunguzwa kwa bajeti ya jumla kutoka shilingi trilioni 4.3, ambapo makadirio mapya yamepunguzwa kwa jumla ya shilingi bilioni 23 kutoka ilivyopangwa awali.

Miongoni mwa taasisi zilizokumbwa na upunguzaji wa bajeti ni Idara ya Ujasusi NIS, ambayo imetengewa shilingi bilioni 51.45 kutoka bilioni 55.65, na Idara ya Uhamiaji na Huduma kwa Raia ambayo sasa itapokea shilingi bilioni 11.77 kutoka bilioni 13.

Hata hivyo, baadhi ya taasisi kama Tume ya Huduma kwa Walimu – TSC – zitapokea fedha zaidi. TSC imeongezewa bajeti kutoka shilingi bilioni 354.6 hadi bilioni 376.9.

Imetayarishwa na Mercy Asami

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *