#Sports

STARLETS MBIONI KUTWA TAJI LA CECAFA

Harambee Starlets wamesalia na mchezo mmoja tu kutwaa ubingwa wa CECAFA kwa Wanawake kufuatia ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Sudan Kusini Uwanja wa Azam Sports Complex jijini Dar es Salaam, Tanzania mnamo Alhamisi.

Ushindi huo uliifanya timu hiyo inayonolewa na kocha Beldine Odemba kuibuka na ushindi wa tatu mfululizo na kuwa kileleni mwa michuano ya timu tano ambayo inachezwa kwa mpangilio wa mzunguko.

Kufuatia ushindi huo mnono, Harambee Starlets wanakaa kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi tisa, tatu juu ya wenyeji Tanzania ambao walikuwa wakicheza na Uganda hadi wakati wa kwenda kwa wanahabari.

Starlets, ambao wanawania taji la pili la kanda mwaka huu, wanakabiliwa na changamoto ngumu zaidi kufikia sasa Jumamosi dhidi ya wenyeji huku mshindi wa duwa hiyo atawazwa mabingwa.

Tanzania imesalia kuwa timu iliyofanikiwa zaidi katika historia ya michuano ya CECAFA kwa Wanawake, ikiwa na mataji mawili, ikilinganishwa na moja la

Imetayrishwa na Nelson Andati

STARLETS MBIONI KUTWA TAJI LA CECAFA

KENYA KUANDAA FAINALI ZA CHAN

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *