JIWE LA STONES YAIOKOLEA CITY ALAMA

Beki wa Uingereza John Stones aliikolea timu yake ya Man City katika dakika za lala salama na kuwapa sare ya mabao 2 dhidi ya Arsenal katika uga wa Etihad.
Man city walichukua uongozi kunako dakika ya 9 kupitia msambuliaji wao matata Erling Halaand baada ya kumegewa pasi na kinda Savino, kabla ya Arsenal kusawazisha Ricardo Calafiori katika dakika 22, huku Gabriel Marghalaes akiwapa uongozi katika dakika za lala salama kwenye kipindi cha kwanza.
Arsenal walilazinika kucheza kipindi chote cha pili wakiwa wachezaji 10 baada ya Loandro Trossard kuonyeshwa kadi nyekundu, ingawa Arsenal wakaonyesha mchezo mzuri kwa kulinda mabao hayo mawili, kabla ya City Kuonyesha ubabe wao na kunyakua pointi moja muhimu katika mchezo huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa