JINSI WAKENYA WATAWAHUSIKA KUTUNGA SHERIA

Kamati ya Fedha na mipango katika bunge la kitaifa imetoa wito kwa Wakenya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kutunga sheria kwa kuwasilisha maoni yao kuhusu mswada wa Fedha wa 2024- 25 kupitia baruapepe au moja kwa moja kwa kamati hiyo.
Katika taarifa kutoka kwa karani wa bunge, hatua hiyo imechukuliwa kisheria ili kuhakikisha uwazi katika mchakato wa kutunga sheria.
Mswada huo unapendekeza marekebisho katika vipengele kadhaa muhimu vya sheria, amabvyo vitaathiri ustawi wa kiuchumi na kifedha kwa wakenya wote.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa