#Local News

ORODHA YA MAWAZIRI WAPYA

Rais William Ruto amefanya uteuzi wa kundi la pili la mawaziri, na kuwateua mawaziri wengine 10 kuhudumu katika baraza lake la mawaziri.

Katika uteuzi mpya, Rais amependekeza mbunge mteule John Mbadi kuhudumu kama Waziri wa fedha, wizara ya michezo Kipchumba Murkomen, Wizara ya Mashirika Wycliffe Oparanya, wizara ya masuala ya kijinsia Stella Lang’at, wizara ya Kawi Opiyo Wandayi ambaye kwa sasa ni mbunge wa Ugunja, Wizara ya utalii Rebecca Miano ambaye wiki jana aliteuliwa kama mwanasheria mkuu, Wizara ya utumishi wa umma Justin Muturi, wizara ya biashara Salim Mvurya, wizara ya Leba Alfred Mutua, naye Hassa Joho akiteuliwa kama Waziri wa madini.

Majina hayo yatawasilishwa katika bunge la kitaifa ili kupigwa msasa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *