SHA YAPIGWA JEKI NA KEMSA

Mpango wa afya ya jamii SHA umepigwa jeki baada ya mamlaka ya kusambaza dawa KEMSA kusambaza vifaa vya kimatibabu kwa serikali za kaunti ili kuimarisha utekelezwaji wa mpango huo katika maeneo ya mashinani.
Vifaa hivyo vikiwemo dawa, vimezinduliwa na Waziri wa afya Deborah Mulongo, akisema kwamba vifaa hivyo vitapiga jeki mpango huo mpya wa afya.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa bodi ya KEMSA Samuel Tunai, amesisitiza umuhimu wa mamlaka hiyo katika utekelezwaji wa mpango wa SHA.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa