KENYA MORAN WATIA FORA

Timu ya Kenya ya mchezo wa raga ya wachezaji saba saba, Kenya Morans, wazidi kutia bidii katika mazoezi wanapojiandaa kwa Mashindano yajayo ya Afrika 7s nchini Mauritius wikendi hii.
Morans wamekuwa katika mazoezi ya pamoja na timu ya, Shujaa, ambao wanaelekea kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris, na kocha msaidizi wa Shujaa Louis Kisia ambaye atachukua mikoba ya Morans nchini Mauritius, anasema hii imefaidi sana timu hiyo.
Kisia ataongoza Morans nchini Mauritius kama kocha mkuu, huku Morgan Ngumbi akiwa meneja wa timu na John Eli akiwa daktari wa kikosi
Shujaa na benchi nyingine ya ufundi watasalia Nairobi kwa mazoezi zaidi, kabla ya kuelekea Miramas, Ufaransa, mwezi ujao kwa michezo ya mwisho kabla ya Michezo ya Olimpiki kuanza.
Kenya wako katika kundi A pamoja na wenyeji Mauritius, Nigeria na Madagascar.
Imetayarishwa na Nelson Andati.