MAKADIRIO YA MAANDAMANO
Watu 22 wanaendelea kuuguza majeraha mbali mbali kutokana na maandamano ya hapo jana katika miji mbali mbali nchini, wakishinikiza kujiuzulu kwa naibu inspekta mkuu wa polisi aliyejiondoa kwa muda Eliud Lagat.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, mwenyekiti wa tume ya kitaifa kuhusu haki za kibinadamu KNHRC Dakta Raymond Nyeris, amesema kati ya majeraha, mengi ya majeraha hayo ni ya risasi, kukatwa kichwani, mijeledi, kugongwa na vifaa but una kuvuta gesi ya kutoa machozi.
Tume hiyo aidha imeshutumu vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano hayo katika miji ya Kilifi, Nairobi, Mombasa na Kwale licha ya polisi kufahamishwa.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































