IAN NJOROGE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMSHAMBULIA POLISI

Dereva mmoja aliyemvamia na kumjeruhi afisa wa polisi wa trafiki huko Mirema jana Jumapili anatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo
Mshukiwa huyo kwa jina Ian Njoroge, amenaswa nyumbani kwake eneo la Jacaranda mtaani Kayole jijini Nairobi wakati wa operesheni iliyoongozwa na maafisa wa upelelezi DCI
Kwa mujibu wa polisi afisa kwa jina Jacob Ogendo alikuwa akidhibiti msongomano wa magari katika barabara hiyo alipolisimamisha gari moja lililokuwa limekiuka sheria za trafiki na liliposimama Ogendo alimwagiza dereva huyo kuandamana nae hadi kituo cha polisi kabla ya kumshambulia.
Imetayarishwa na Janice Marete