LUSAKA AONYA WAKULIMA DHIDI YA KUUZA PEMBEJEO ZA RUZUKU
Wakulima wa Bungoma wameonywa dhidi ya kuuza pembejeo za kilimo zilizopewa ruzuku na serikali ya kaunti badala ya kuzitumia ipasavyo.
Gavana Kenneth Lusaka amesema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaopatikana wakikiuka mpango huo, ambao unalenga kusaidia wakulima wadogo wakati wa msimu wa upanzi.
Aidha, amethibitisha kuwa maandalizi ya usambazaji wa pembejeo za bure kwa mwaka huu yanaelekea kukamilika na kuwataka wakulima kuzitumia kwa ufanisi ili kuimarisha usalama wa chakula.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































