WAKAAZI WA KAUNTI YA TRANSNZOIA WALALAMIKIA KUBAGULIWA KATIKA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA TRANSNZOIA-SEBIT

Wakaazi wa kaunti ya Pokot magharib wameandamana kulalamikia kubagulia katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Transnzoia -Sebit.
Wakazi hao wameitaka kampuni ya uchina ambayo inaendeleza ujenzi wa barabara hiyo kutokuwa na upendeleo wakati wa kutoa nafasi za ajira.
Mwakilishi wa wadi ya Mnagei Richard Todosia ametoa wito kwa uongozi wa kampuni hiyo kushughulikia malalamishi ya wakaazi.
Naye mwakilishi ya wadi ya Sitatunga ya kaunti jirani ya Transnzoia Simon Murrey amepuuzilia mbali madai hayo akiyataja kuwa ya uongo.
Imetayarishwa na Janice Marete