MWANAMUME WA MIAKA 25 AFARIKI JIKONI KWA MAMAYE SIAYA

Polisi katika kaunti ya Siaya wameanzisha uchunguzi kufuatia kifo cha mkazi mmoja huko Ugenya.
George Nyaginde Amenya mwenye umri wa miaka 25 amepatikana amefariki jikoni kwa mamake.
Inaarifiwa kuwa marehemu alivamiwa katika kitongoji cha Nyalenya kilichopo Uyunya.
Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Siaya Cleti Kimaiyo, kisa hicho kiliripotiwa katika kituo cha polisi cha kushika doria cha Aboke.
Imetayarishwa na Janice Marete