#Local News

RAIS WA IRAN EBRAHIM RAISI AFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE

Rais wa Iran Ebrahim Raisi amefariki dunia kutokana na majeraha aliyopata hapo jana baada ya ndege aina ya helikopta aliyokuwa ameabiri kuanguka katika eneo la milimani nchini humo.


Haya ni kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo ila Serikali ya Iran bado haijatoa uthibitisho wa kifo cha kiongozi huyo.


Vikosi vya uokoaji vimekuwa vikizunguka eneo hilo tangu Jumapili mchana baada ya helikopta iliyokuwa imembeba Raisi, waziri wa mambo ya nje na maafisa wengine kupata ajali.

Imetayarishwa na: Janice Marete.

TUSIHUSISHE WATOTO WA SHULE KATIKA MAPENZI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *