POLISI WAMKAMATA DEREVA ALIYEMSAFIRISHA MUUAJI WA MBUNGE WERE

Polisi wanaendeleza uchunguzi baada ya kumkamata Amos Barasa Kasili, dereva wa bodaboda anayedaiwa kumsafirisha mshukiwa aliyempiga risasi Mbunge wa Kasipul Charles Were mnamo Aprili 30.
Kasili amekamatwa Kibera baada ya uchunguzi wa kielelezo kuthibitisha uwepo wake eneo la tukio.
Pikipiki yake inalingana na ile iliyorekodiwa kwa CCTV ikifuatilia gari la mbunge huku DCI ikihusisha mauaji hayo na mtandao wa kihalifu wenye uwezo wa kifedha.
Imetayarishwa na Janice Marete