#Local News

POLISI WACHUNGUZA MAUAJI KWA MOTO HUKO KAKAMEGA

Polisi wanachunguza kifo cha mwanamke mwenye umri wa miaka 38 aliyechomeka hadi kufa katika kisa kinachoshukiwa kuwa ni tukio la uhalifu katika kijiji cha Malinya, Ikolomani, Kaunti ya Kakamega.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo huku majirani wakidai kuwa mlango wa nyumba hiyo ulikuwa umefungwa kutoka nje, jambo linaloashiria uwezekano wa njama.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika hifathi ya Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kakamega huku uchunguzi ukiendelea.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *