#International

UKRAINE TAYARI KUZUNGUMZA NA URUSI- TRUMP

Huenda vita ambavyo vimedumu kwa miaka 3 kati ya Urusi na Ukraine vikafikia kikomo baada ya rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kutangaza kwamba yuko tayari kwa mazungumzo na Urusi na ukamilishaji wa mkataba wa uchimbaji madini na serikali ya Marekani.

Hatua ya Zelensky kukubali mazungumzo imewekwa wazi na mwenzake wa Marekani Donald Trump, ambaye amethibitisha kupokea waraka kutoka kwa Zelensky, unaosema nikinukuu, “Ukraine iko tayari kuja kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kupata mwafaka wa kudumu wa amani. Hakuna anayetaka amani Zaidi ya raia wa Ukraine.” Mwisho wa nukuu.

Tangazo hili linajiri siku chache baada ya Trump na Zelensky kurushiana cheche za maneno mbele ya wanahabari katika Ikulu ya White House.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UKRAINE TAYARI KUZUNGUMZA NA URUSI- TRUMP

NANDI, RED CROSS ZASHIRIKIANA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *