#Business

SERIKALI IMEZINDUA MPANGO WA KUBORESHA BIASHARA YA NJE YA NCHI

Serikali kuu imezindua mpango unaolenga kupiga jeki biashara ya nje ya nchi kwa asilimia 10 kwa mwaka kutoka shilingi trilioni moja zilizorekodiwa mwaka jana.

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Biashara za Nje Jaswinder Bedi amesema kuwa mpango huo unatumika kama ramani ya kulifanya taifa la Kenya kuwa nchi ya uchumi unaoongozwa na biashara ya nje na kutambulika kote duniani

Bedi Ameongeza kuwa, mpango huo unatoa utaratibu utakaowezesha serikali kupanua biashara yake ndani ya bara la Afrika, ambalo ni soko kubwa la nchi hii, kwa kuongoza katika utekelezaji kamili wa Eneo la Biashara Huria la Afrika.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *