JOHO AWAONYA WANYAKUZI WA MAENEO YA UVUVI
Waziri wa madini na uchumi wa raslimali za majini Hassan Joho, amewaagiza wanyakuzi wa maeneo ya uvuvi katika maeneo mbali mbali nchini kuondoka mara moja.
Akizungumza jijini Mombasa, Joho amesema kwamba tayari awaagiza magavana kutoka kaunti ambako shughuli za uvuvi huendelea kushirikiana na makamishna wa kaunti hizo kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa.
Aidha, Waziri Joho amesema wizara yake imejiandaa kisawasawa kukabili suala la uvuvi haramu katika bahari Hindi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































