#Sports

INZAGHI AWAPUZULIA MBALI WAKOSOAJI

Kocha wa zamani wa Inter Milan Simone Inzaghi amepuuzilia mbali ukosoaji wake kuhusu namna alivyohamia klabu ya Al-Hilal ya Saudia.

Inzaghi anaanza kuinoa klabu yake mpya kwa mara ya kwanza Jumatano watakapomenyana na Real Madrid katika Kombe la Dunia la Vilabu huko Miami.

Afisa mkuu mtendaji wa Al-Hilal Esteve Calzada aliambia BBC Jumatano kwamba hatua hiyo iliamuliwa kabla ya Inter kushindwa kwa mabao 5-0 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Paris Saint-Germain. Fainali ya Ligi ya Mabingwa ilifanyika Mei 31 na Inzaghi alitangazwa kuwa kocha wa Al-Hilal siku nne baadaye.

Katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi, Inzaghi aliulizwa kuhusu ripoti hizo.

Najua nitaikosa, nitakosa kila kitu, hata hii. Hata tuhuma zisizo za haki ambazo zimetolewa kwa miaka minne iliyopita.

“Lakini nimekuwa na furaha sana, nimejitolea na kufanya kazi kwa karibu na klabu na uongozi. Kwa kifupi, nadhani wao pia, kwa manufaa ya Inter, waliamini kuwa jambo sahihi la kufanya ni njia zetu kutengana, na maumivu mengi kwa upande wa kila mtu,” alisema.

Inzaghi alitetea chaguo lake la kuhama kutoka klabu kubwa ya Ulaya hadi Ligi inayoibuka ya Saudi Pro League.

“Nilikubali changamoto na kujiondoa kwenye eneo langu la starehe baada ya miaka kadhaa ndani ya Inter. Nataka kubadilisha njia yangu ya kufikiri, mtindo wangu wa uchezaji, na kujaribu mambo mapya. Hakukuwa na timu nyingine nilitaka kuifundisha. Kwa hivyo nilichagua Al Hilal,” aliongeza.

Imetayrishwa na Nelson Andati

INZAGHI AWAPUZULIA MBALI WAKOSOAJI

KNH ILIPOKEA MAJERUHI 16 WA MAANDAMANO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *