NYONG’O APINGA MSWADA UNAOWAZUIA MAGAVANA WALIOSTAAFU KUGOMBEA VITI VYA UBUNGE

Gavana wa Kaunti ya Kisumu Anyang Nyong’o amelitaka Bunge la Seneti kuondoa Mswada wa Marekebisho ya Katiba ya Kenya wa 2023, unaolenga kuwazuia magavana wa zamani kugombea nyadhifa zingine za uchaguzi.
Mswada huo unalenga kuwafungia magavana baada ya kutumikia muhula wao wa miaka 10 afisini.
Nyong’o anasema mswada huo ni kinyume cha katiba kwa kuwa utakiuka haki yao ya kugombea nyadhifa za kuchaguliwa kama ilivyoainishwa chini ya Kifungu cha 38 cha Katiba.
Nyong’o amesema Seneti inafaa kuipa kipaumbele Miswada inayoimarisha ugatuzi, ambayo kulingana naye iko hatarini, badala ya kuzingatia siasa za bei nafuu.
Nyong’oambaye pia amewahi kuhudumu kama Seneta wa kaunti ya Kisumu kwa maka mitano anadai kuwa hakuna mwanasiasa anayefaa kuzuiwa kutekeleza haki zake, bila kujali wadhifa wake wa zamani, na kuongeza kuwa mafanikio ya demokrasia, kama ilivyoainishwa katika Katiba, lazima yaheshimiwe.
Imetayarishwa na Janice Marete