RAIS MADURO AKIMBIA IKULU

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametoroka kutoka ikulu yake kutokana na maandamano makali ya kupinga uchaguzi wake, waandamanaji wakisafiri kutoka kilomita kadhaa na kutishia kuvamia ikulu hiyo.
Mapema leo, vikosi vya usalama vimetumia risasi za mipira na vitoza machozi kuwakabili waandamanaji.
Vurugu zimeanza katika jiji kuu la Caracas baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza Maduro kuwa mshindi kwneye uchaguzi ulioandaliwa Jumapili dhidi ya mwaniaji wa upinzani Edmundo Gonzalez
Imetayarishwa na Antony Nyongesa