#Football #Sports

HUSSEIN MOHAMMED APUUZILIA BARUA YA FKF

Hussein Mohammed amepuuzilia mbali barua ya mkurugenzi mtendaji wa FKF Barry Otieno akidai kuwa yeye si makamu mwenyekiti halali wa klabu ya Muranga Seal inayoshiriki kwenye ligi kuu soka nchini FKF.

Mohammed, alisema FKF haina uwezo wa kuamua ni nani atateuliwa na klabu ya ligi kuu, akitaja hatua ya FKF kuwa haramu na isiyo na maana.

Haya yanajiri baada ya Otieno kukataa ombi la Seal la kutaka Mohammed awe mwakilishi wao katika mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo uliopangwa kufanyika Machi mwaka huu, akisema kuwa hajasajiliwa kama mwanachama wa klabu hiyo.

Wakati uo huo Hussein ametoa wito kwa haja ya kuhakikisha kesi zote zinazosalia mahakamani zinazohusu FKF zimetatuliwa ili kuandaa uchaguzi wa shirikisho.

Imetayrishwa na Nelson Andati

HUSSEIN MOHAMMED APUUZILIA BARUA YA FKF

ANDUGU ANA MATUMAINI YA MSIMU UJAO

HUSSEIN MOHAMMED APUUZILIA BARUA YA FKF

MKATABA WA MBAPPE NA REAL MADRID

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *