#Local News

MVULANA AJIUA BAADA YA KUZUIWA KUUZA NG’OMBE BILA IDHINI YA BABA YAKE

Polisi katika Kaunti ya Migori wanachunguza kifo cha mvulana wa umri wa miaka 17, ambaye anadaiwa kujiua saa chache baada ya kuzuiwa kuuza ng’ombe wa babake kwenye mnada wa ng’ombe katika kijiji cha Mawini.

Chifu Msaidizi wa eneo la Nyamaharaga Rose Ooko amesema mwili wa marehemu umepatikana ukining’inia kwa kamba ndani ya kichaka saa chache baada ya kuzuiwa kuuza ng’ombe huyo bila kitambulisho cha kitaifa cha babake.

Baada ya kugundua kuwa hangeweza kuuza ng’ombe huyo bila kitambulisho cha kitaifa cha babake, Ooko aidha ameongeza kuwa marehemu ameomba usimamizi wa mnada wa ng’ombe kumruhusu kukimbia nyumbani na kuleta hati hiyo lakini hakurejea. Ndiposa wakawa na wasi wasi wakaanza kumtafuta na kuupata mwili wake.

Chifu amesema bado hawajajua ni nini kilimlazimisha kijana huyo kujitoa uhai ingawaje amehoji iwapo mtoto huyo angejiua kwa kuhofia kwamba babake atamchukulia hatua za kinidhamu kwa kujaribu kuuza ng’ombe bila ruhusa yake.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Migori Level Four ukisubiri uchunguzi.

Imetayarishwa na Janice Marete

MVULANA AJIUA BAADA YA KUZUIWA KUUZA NG’OMBE BILA IDHINI YA BABA YAKE

WAHUDUMU WA AFYA WATAKA MALIPO YA MISHAHARA

MVULANA AJIUA BAADA YA KUZUIWA KUUZA NG’OMBE BILA IDHINI YA BABA YAKE

UPASUAJI WA MIILI YA WANAFUZI 21 WALIOAGA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *