SABABU ZA KUKATALIWA KWA SOI KUWA WAZIRI

Wabunge wanaendelea kujadili ripoti kuhusu mawaziri wateule ambao walipigwa msasa, ripoti hiyo ikiwasilishwa leo bungeni na kamati ya uteuzi.
Mjadala mkali umeendelea bungeni humo kuhusiana na kamati hiyo kukataa kuidhinisha uteuzi wa Stella Soi ambaye alikuwa ameteuliwa kuhudumu kama Waziri wa jinsia.
Hata hivyo, kiongozi wa walio wengi bungeni humo Kimani Ichung’wa, ameweka wazi sababu za kamati hiyo kudinda kuidhinisha uteuzi wa Soi, ikiwemo ukosefu wa tajriba katika masuala ya usimamizi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa