RACHIER KUWANIA TENA UENYEKITI WA GOR MAHIA
Mwenyekiti wa Gor Mahia, Ambrose Rachier, atawania tena kiti chake katika uchaguzi wa klabu utakaofanyika Aprili 13, 2025, sambamba na Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) katika Uwanja wa Nyayo.
Amesema ana haki ya kugombea kwa mujibu wa katiba ya klabu na uamuzi wa Mahakama ya Michezo, huku akipuuza wakosoaji wake.
Uchaguzi huo, uliocheleweshwa kwa migogoro ya ndani, utasimamiwa na IEBC, na wagombea wanapaswa kutimiza vigezo vya Msajili wa Michezo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































