SERIKALI YAKODISHA VIWANDA VYA SUKARI ILI KUFUFUA SEKTA YA SUKARI
Serikali imeanzisha hatua mpya ya kufufua sekta ya sukari nchini kwa kukodisha viwanda vinne vya sukari kwa kipindi cha miaka 30 vilivyokuwa vikikumbwa na changamoto kubwa za kifedha.
Kampuni ya Kibos Sugar and Allied Industries Limited imechukua usimamizi wa Chemelil Sugar, Muhoroni Sugar Factory sasa iko chini ya West Valley Sugar Company, West Kenya Sugar Company, chini ya uongozi wa Jaswant Rai, imechukua Nzoia Sugar, na Busia Sugar Industry imeanza kusimamia Sony Sugar.
Waziri wa biashara ndogo ndogo na za kati, Wycliffe Oparanya, amesisitiza kuwa viwanda hivyo vimekuwa vikikumbwa na hasara kubwa kwa miaka mingi, vikiwa vinatumia vifaa vya zamani ambavyo vimekuwa vikizorotesha uzalishaji.
Imetayarishwa na Mercy Asami
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































