WAZEE WA MITAA KUJUA HATMA

Hatma ya wasimamizi wa vijiji kuanza kupokea malipo yao ya kila mwezi itabainika hivi karibuni kutokana na maoni yatakotolewa na wakenya kwenye vikao vya ukusanyaji wa maoni vinavyoongozwa na wizara ya usalama wa kitaifa.
Vikao hivyo vitaandaliwa hapo kesho katika kaunti 10 ikiwemo Kakamega, Nairobi, Uasin Gishu, Nakuru, Mombasa na Machakos.
Kwenye pendekezo hilo, wazee hao ambao kwa sasa wanafahamika kama village elders, watapewa wadhifa wa village administrative elders.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa