MAHAKAMA YAMWAMRISHA IG KANJA KUMWASILISHA BLOGA NDIANGUI

Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja ameagizwa na mahakama kuonyesha aliko bloga Ndiangui Kinyangia aliyetoweka siku 10 zilizopita.
Kwenye uamuzi wake, jaji Chacha Mwita amemtaka Kanja kumwasilisha bloga huyo mahakamani bila kukosa au aseme ni kwanini hawezi kupatikana kifikia kesho saa tano asubuhi.
Suala hilo litatajwa tena kesho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa