HOJA YA KUKOSA IMANI KWA RUTO YAFIKA SENETI

Seneta wa Makueni Dan Maanzo amewasilisha katika bunge la seneti mswada wa kukosa imani na Rais William Ruto, wakati ambapo tayari mswada wa kumbandua naibu wake Rigathi Gachagua umewasilishwa katika bunge la kitaifa.
Kwenye mswada huo, Maanzo ameorodhesha ukosefu wa usalama katika maeneo mengi ya nchi na mauaji ya waandamanaji wakati wa maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z kama vigezo vya kumtimua Rais Ruto.
Aidha, mbali na madai ya Rais Ruto kushindwa kuwalinda wakenya, seneta Maanzo amemshutumu kwa madai ya kutekeleza mageuzi yasiyofaa katika sekta za elimu na afya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa