WALIMU WAANDAMANA NAIROBI, WAAPA MGOMO UNGALIPO

Walimu wa shule za sekondari wamelemaza masomo kwa siku ya 5 mfululizo kote nchini wakiitaka tume ya kuwaajiri walimu TSC itekeleze mkataba wa maelewano wa kati ya mwaka 2021-25 ikiwemo kuwapa makataba wa kudumu walimu wa JSS.
Jijini Nairobi, walimu hao wameandamana hadi katika afisi za TSC wakisisitiza kwamba mgomo utaendelea hadi mkataba wao utekelezwe.
Aidha, muungano wa walimu hao KUPPET umeikosoa TSC kwa kuwataka waandike barua ya kuitisha mazungumzo na kisha kuichapisha barua hiyo mitandaoni.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa