BADO HATUELEWANI NAIBU GAVANA ODUOL ASEMA
Naibu gavana wa kaunti ya Siaya William Oduol ameiambia kamati ya ugatuzi katika bunge la seneti kwamba uhusiano wake na gavana James Orengo umedorora tangu jaribio la kubanduliwa kwake mwezi juni mwaka jana.
Amesema kwamba mara kwa mara serikali ya kaunti hiyo imemhujumu kwa kukosa kumpa marupurupu yake na fedha zingine za kumwenzesha kutekeleza majumu yake.
Kamati hiyo hata hivyo imeahidi kusikiliza upande wa gavana Orengo kabla ya kujaribu kuwapatanisha.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































