#Local News

BLOGA NDIANG’UI APATIKANA

Bloga Ndiang’ui Kinyagia, aliyeripotiwa kutoweka yapata wiki 2 zilizopita, amewasiliana na familia yake na kuthibitisha kwamba yuko hai na salama.

Kulingana na taarifa ya wakili wa familia yake Wahome Thuku, Kinyagia aliwasiliana na mwanafamilia Jumanne jioni ila hakufichua alikokuwa, akifichua kuwa alielekea mafichoni baada ya kubaini kuwa alikuwa akitafutwa na maafisa wa DCI.

Haya yanajiri huku mkurugenzi wa DCI Mohammed Amin akiratibiwa kumwasilisha bloga huyo mahakamani kabla ya saa tano hii leo jinsi alivyoagizwa na jaji Chacha Mwita.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

BLOGA NDIANG’UI APATIKANA

HATUMTAKI DIAZ WAEMA LIVERPOOL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *