KUPANDA KWA BEI YA VYAKULA VYA MIFUGO KUNACHANGIWA NA UKOSEFU WA MALI GHAFI

Watengenezaji wa lishe ya mifugo wanasema kuwa ukosefu wa mali ghafi ya kutengeneza vyakula hivyo umesababisha kupanda kwa bei ya chakula cha mifugo.
Mwenyekiti wa muungano wa watengenezaji wa lishe ya mifugo joseph Karuri anasema muungano huo uagiza zaidi ya asilimia 70 ya mali ghafi kama vile soya, sunflower na mahindi kutoka kwa mataifa ya nje ya nchi jambo ambalo uchangia bei ghali ya vyakula hivyo humu nchini.
Imetayarishwa na Janice Marete