POLISI WAONYA DHIDI YA ‘KUJILINDIA’ BIASHARA
Idara ya polisi imewaonya wafanyabiashara kuwakodisha vijana kuwalindia biashara wakati wa maandamano na badala yake wakatakiwa kuwaruhusu maafisa wa polisi kutekeleza jukumu hilo.
Kupitia taarifa, msemaji wa polisi Muchiri Nyaga ameonya kuwa hatua hiyo ni kinyume na sheria, akisisitiza kuwa ni jukumu la polisi kuhakikisha usalama wa mali, na uharibifu wa aina yoyote utakabiliwa kisheria.
Taarifa yake inajiri kufuatia maandamano ya wiki jana ambako ilirpotiwa kuwa baadhi ya wanasiasa waliwapa rungu vijana kuzua rabsha kwa kisingizio cha kulinda biashara.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































