ZIWA TURKANA LAVUNJA KINGO ZAKE

Baadhi ya wakaazi katika kaunti ya Turkiana wanaoshi karibu na ziwa Turkana wameachwa bila makao baada ya Ziwa Turkana kuvunja kingo zake na kuathiri makaazi yao.
Mbunge wa Turkana ya kati Namuar Joseph Emathe amesema kuwa kufurika kwa ziwa hilo ni mojawapo ya athari za mabadiliko ya hali ya anga na kwamba kuna baadhi ya wafugaji katika sehemu nyingine ambao pia wamepoteza mali yao na mifugo wao kufa kutokana na kiangazi.
Imetayarishwa na Janice Marete