SIOYI, FATUMA WASHUTUMU DHULUMA ZA KIJINSIA

Mwakilishi wa kike katika kaunti ya Trans nzoia Lilian Sioyi na mwenzake wa Migori Fatuma Mohammed, wamelalamikia ongezeko la visa vya dhuluma dhidi ya akina mama hasa wajane.
Wakizungumza wakati wa kuwapa akina mama vifaa vya kuwainua kiuchumi, viongozi hao wamehimiza ushirikiano na idara ya usalama kama njia mojawapo ya kukabili visa hivyo.
Hafla hiyo aidha imehunduriwa na mbunge wa Kiminini kakai Bisa una seneta wa Trans Nzoia Allan Chesang ambao wamehimiza utumizi mwafaka wa vifaa hivyo vya msaada.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa