WIZARA YA AFYA KUZINDUA MAFUNZO NCHINI KOTE KABLA YA KUANZISHWA KWA SHA

Wizara ya Afya inazindua mafunzo kote nchini kabla ya kuanzishwa rasmi kwa huduma za Mamlaka ya Afya ya Jamii.
Uzinduzi huo utaongozwa na Waziri wa Afya Deborah Barasa ambapo ataungana na katibu wa Huduma za Matibabu Harry Kimtai, Mkurugenzi Mkuu wa Afya Patrick Amoth, na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Afya ya Jamii na Mkurugenzi Mtendaji.
Huduma hizo zitaanza kutumika kikamilifu ifikapo Oktoba 1, wakati watumishi wote wa umma watakapoelekezwa kuwa wamejiandikisha kwenye Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (SHIF).
Haya yanajiri siku chache baada ya msemaji wa serikali Isaac Mwaura kusema serikali inaangazia uhamasishaji na elimu kwa umma kuhusu mabadiliko kutoka NHIF hadi SHA.
Imetayarishwa na Janice Marete