MAHAKAMA YA LEBA YAWATAKA WAHADHIRI WA VYUO VIKUU KUSITISHA MGOMO WAO NA KUSHIRIKI MAZUNGUMZO

Mahakama ya leba imetangaza mgomo unaoendelea wa wahadhiri kuwa hauna ulinzi ikiwataka maafisa wake kurejea kwenye meza ya mazungumzo.
Wahadhiri chini ya Muungano wa Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu (UASU) wameanza mgomo wa jana Jumanne wakiitaka serikali kuzingatia matakwa yake kama ilivyoainishwa katika Makubaliano ya Pamoja ya Majadiliano ya 2012-2025 (CBA).
Kwa hivyo mahakama imewataka wafadhili kukaribisha mazungumzo na serikali ili kutoa nafasi ya kuunda fomula inayofaa ya kurejea kazini.
Imetayarishwa na Janice Marete