#Football #Sports

AMADOU AJIUNGA NA VILLA

Aston Villa wamemsajili kiungo Amadou Onana kutoka Everton kwa mkataba wa £50m.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alicheza kila dakika ya kampeni ya Ubelgiji ya Euro 2024 na sasa ana fursa ya kuiwakilisha Villa kwenye Ligi ya Mabingwa ulaya ya msimu ujao.

Onana alijiunga na Everton kutoka Lille kwa £33m mwaka 2022 na alicheza mechi 72 akiwa na The Toffees, akifunga mabao manne.

Alihusishwa na kuhamia Arsenal mnamo 2023, na vilabu vingi vikubwa viliripotiwa kumuwinda.

Mkufunzi wa Villa Unai Emery alikuwa akitafuta kiungo mpya wa kati baada ya klabu hiyo kumuuza Douglas Luiz kwenda Juventus kwa £42.35m mwezi Juni.

Onana alisema kuwa kiungo wa Villa na mchezaji mwenzake wa Ubelgiji Youri Tielemans alimshawishi kujiunga na klabu hiyo ya Midlands.

Kuwasili kwa Onana kumeifanya Villa kutumia hadi takriban £140m kwenye dirisha hili la uhamisho.

Villa pia wametumia £35m kumsajili Ian Maatsen kutoka Chelsea, £18.6m kuwanasa Samuel Iling-Junior na Enzo Barrenechea kutoka Juventus, £18m kwa Jaden Philogene kurejea kutoka Hull, £5m kumnunua Ross Barkley kutoka Luton na £9m kwa uhamisho wa Lewis Dobbin kutoka Everton.

Wataanza kampeni yao ya Ligi ya Premia huko West Ham Jumamosi, 17 Agosti.

Imetayarishwa na Nelson Andati

AMADOU AJIUNGA NA VILLA

TUTAOGELEA KWA USHINDI KULE PARIS

AMADOU AJIUNGA NA VILLA

WANA BUNDUKI WAKO MBIONI KUMSAJILI RICCARDO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *