MAGARI 26, PIKIPIKI 18 ZACHOMWA NYANDARUA- SERIKALI
Uharibifu zaidi wa mali ya serikali na ya kibinafsi imeendelea kuripotiwa nchini, siku moja baada ya maandamano ya kuwakumbuka waathiriwa wa maandamano ya mwaka jana.
Katika kaunti ya Nyandarua, serikali ya kaunti hiyo imeripoti kuchomwa moto kwa magari yake 26 yaliyokuwa yameegeshwa katika afisi za kaunti ndogo ya Olkalou.
Aidha, imesema pikipiki zake 18 zilichomwa, Pamoja na kifaa cha muziki kilichonunuliwa maajuzi.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































