WATAKAOCHAFUA MAZINGIRA WATAKABILIWA KWA MUJIBU WA SHERIA
Wito umetolewa kwa watu ambao wanahatarisha Maisha ya wakenya kwa kuchafua mazingira kukoma mara moja.
wizara ya mazingira imesema kuwa itachapisha rasmi kwenye gazeti la serikali sheria mpya zitakazotumika na viwanda ili kukabili tatizo la uchafuzi wa mazingira.
Waziri wa mazingira Aden Duale amesema kuwa viwanda vitakavyokiuka sheria hizo na kuhatarisha Maisha ya wakenya vitawajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































