NAIBU GAVANA KERICHO AIBUA MADAI YA UFUJAJI
Naibu Gavana wa Kaunti ya Kericho, Fred Kirui ameibua madai ya kufujwa kwa zaidi ya shilingi milioni 80 katika serikali ya kaunti hiyo, akitaka uchunguzi kufanywa na kuwawajibisha wahusika.
Kirui ambaye amekuwa na utofauti na Gavana Eric Mutai, amesema pesa hizo zililipwa kwa zaidi ya kampuni 33 za kandarasi na usambazaji bidhaa.
Anadai kuwa malipo hayo yalifanyika kati ya Oktoba mwaka jana na Aprili mwaka huu ila bidhaa hizo hazikuwasilishwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































