DUALE: MSWADA WA KUONGEZA MUHULA WA URAIS HAUTAFAULU

Waziri wa Mazingira Aden Duale sasa anasema azma ya kuongeza muhula wa urais kutoka miaka mitano ya sasa hadi miaka saba haitafanikiwa.
Duale amewahakikishia Wakenya kwamba hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu Mswada huo, ambao umeibuliwa na Seneta wa Nandi Samson Cherargei.
Mswada huo pia unahusu kuongezwa kwa kikomo cha muda kwa wawakilishi wadi, wabunge, magavana na maseneta, kwa kurekebisha vifungu vya vya katiba.
Akizungumzia Mswada huo Duale ameonyesha imani kuwa mabunge mengi hayatauunga mkono mswada huo.
Imetayarishwa na Janice Marete