MWANARIADHA WA UGANDA REBECCA CHEPTEGEI AFARIKI DUNIA
Mwanariadha wa uganda Rebecca Cheptegei amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Moi mjini Eldoret alipokuwa akipokea matibabu kutokana na majeraha ya moto aliyopata baada ya kushambuliwa na mpenzi wake wa zamani.
Cheptegei ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 33.
Kaimu Mkurugenzi wa hosipitali ya Moi Dkt Owen Menach amethibitisha kufariki kwake usiku wa kuamkia leo baada ya viungo vyake kufeli.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































