MUNYA;RAILA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI NI LENGO LA KUJINUFAISHA KISIASA

Kiongozi wa chama cha PNU Peter Munya ameendelea kukosoa hatua ya chama cha ODM ambacho ndicho chama tanzu cha mrengo wa azimio kwa kushirikiana na serikali.
Munya amekiri kuwa mapatano ya rais Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga ni kwa lengo la kujilinda kisias baada ya maandamano ya vijana wa gen-z kuleta mabadiliko makubwa.
Ameongeza kuwa rais Ruto na Raila Odinga wameungana ili kuthibiti mashinikizo ya vijana wa Gen-Z.
Imetayarishwa na Janice Marete