#Local News

KMA YATOA MAKATAA KWA SERIKALI KUTATUA MZOZO KUHUSU KODI YA LESENI ZA HOSPITALI

Muungano wa madaktari Kenya Medical Association umetoa makataa ya wiki mbili kwa baraza la mawaziri na serikali ya kitaifa ,kufanya mazungumzo na kutoa mwelekeo wa iwapo serikali zote za ugatuzi zitaendelea kuzitaka hosipitali kulipa kodi ya leseni ya kuhudumu ama la.

Naibu wa rais wa muungao huo Dkt Ibrahimu Matende amesema kuwa baada ya wiki mbili kukamilika na mwelekeo kukosa kutolewa, hospitali za umma zitasitisha huduma hizo.

Matende aidha ameongeza kuwa serikali za ugatuzi kwa muda sasa zimekuwa zikilazimisha hospitali za binafsi kulipa kodi hiyo ambayo kulingana naye ni kinyume na sheria ikizingatiwa kwamba zimekuwa zikilipa ada ya kuhudumu kwa KMA.

Imetayarishwa na Janice Marete

KMA YATOA MAKATAA KWA SERIKALI KUTATUA MZOZO KUHUSU KODI YA LESENI ZA HOSPITALI

KAUNTI ZAPUNGUZIWA MGAOMGAOKAUNTI ZAPUNGUZIWA MGAO

KMA YATOA MAKATAA KWA SERIKALI KUTATUA MZOZO KUHUSU KODI YA LESENI ZA HOSPITALI

VIONGOZI WAMTAKA RAIS RUTO KUFUTILIA MBALI SHA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *